Haji Manara amaliza kila Kitu ishu ya Yondani kutajwa Simba

Haji Manara amaliza kila Kitu ishu ya Yondani kutajwa Simba

0

Haji Manara amaliza kila Kitu ishu ya Yondani kutajwa Simba

Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara ameamua kumaliza kila kitu juu ya Taarifa zinazoenea kuhusu Kelvin Yondani kutua Simba.

Wakati wengi wakiaminishwa kuwa Kelvin Yondani amesaini miaka 2 Simba, Haji Manara amekanusha Taarifa hizo na kusema kuwa hiyo ni Janja ya Yanga ya kuwatuliza Washabiki wake baada ya matokeo ya leo dhidi ya Gor Mahia akiamini Yanga watafungwa.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Haji Manara anaamini Yanga wametunga Hii Story ili baadae wamalizane na mchezaji huyo na Kisha waoneakane Simba walimtaka ila wao (Yanga) ndiyo wamemalizana naye.

” Narudia tena na tena hii taarifa imetungwa ili baadae ionekane Simba walimtaka kisha Mbute wakamdaka ..hii movie inatengenezwa ili kuwapoza washabiki wao kwa kitakachotokea leo Nairobi..tumewashtukia!! Simba ishavuka huko “

Ameandika Manara kupitia Instagram yake

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY