Hawa ni Wachezaji watatu waliofanikiwa kuongezewa Mikataba Yanga

Hawa ni Wachezaji watatu waliofanikiwa kuongezewa Mikataba Yanga

0

Hawa ni Wachezaji watatu waliofanikiwa kuongezewa Mikataba Yanga

Jana Klabu ya Yanga ilifanikiwa kumalizana na wachezaji wake watatu ambao walikuwa wamemaliza mkataba ndani ya Yanga.

Wachezaji hao walifika jana makao makuu ya Klabu ya Yanga kwaajili ya Zoezi hilo ambalo washabiki wengi wa Yanga walikuwa wanatamani kuona Yanga ikifanikisha kuongezea mikataba wachezaji wake waliomaliza Mikataba yao.

Wachezaji ambao Yanga imefanikiwa kuwabakiza Klabuni hapo baada ya Mikataba yao Kuisha ni Kipa Beno Kakolanya ambaye hakuwa na msimu mzuri sana msimu uliopita kutokana na kuandamwa na majeraha lakini sasa hali yake imekaa sawa.

Wachezaji wengine ni Juma Abdul ambaye ni beki wa Kulia mwenye sifa ya Kupiga krosi kali na Beki wa Kati Andrew Vincent.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY