Hii hapa Cv ya kocha mpya Simba aliyetambulishwa jana

Hii hapa Cv ya kocha mpya Simba aliyetambulishwa jana

0

Hii hapa Cv ya kocha mpya Simba aliyetambulishwa jana

July 19 klabu ya Simba ilimtambulisha kocha wake mkuu, Mbelgiji Patrick Aussems kurithi mikoba iliyoachwa na mfaransa, Pierre Lechantre. Kocha huyo ambaye alikua akitumika katika nafasi ya ulinzi enzi za uchezaji wake katika vilabu mbalimbali vya nchini Ubelgiji na nchini Ufaransa alikoaanzia kazi yake ya ukocha.

Akiwa nchini Ubelgiji kocha huyo alicheza kwenye timu za RCS Vise, Standard de  liege, K.A.A Gent na RFC Seraing na hatimaye kutimkia kunako klabu ya ES Troyes Ac ambayo inashiriki ligi kuu nchini Ufaransa.

Akiwa Ufaransa alicheza katika klabu moja pekee na kisha kuanza kuinoa klabu hiyo mnamo mwaka 1992. Kocha huyo mwenye miaka 53 amefanikiwa pia kuvinoa vilambu mbalimbali Afrika vikiwemo vilabu vya AC Leopards na Al Hilaly. Aidha amepata nafasi ya kuzifundisha timu za za taifa ambazo ni timu ya taifa ya Nepal na Benin akiwa kama kocha mkui na Mkurugenzi wa Ufundi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY