Kaheza Apewa Majukumu Ya Kumkalisha Okwi Benchi

Kaheza Apewa Majukumu Ya Kumkalisha Okwi Benchi

0
Kaheza Apewa Majukumu Ya Kumkalisha Okwi Benchi.
Mshambuliaji mpya wa Simba, Marcel Kaheza amedai kufurahia majukumu aliyopewa na Kocha wake, Masoud Djuma, ambaye ameamua kumtumia kama winga badala ya mshambuliaji wa kati, nafasi aliyokuwa akiicheza alipokua Majimaji ya Songea.

Mchezaji huyo aliyeng’ara kwenye kikosi cha Simba kilichotinga robo fainali ya michuano inayoendelea ya Kombe la Kagame, alisema anafurahia kucheza nafasi hiyo na imemfanya kujiamini zaidi uwanjani.

Kaheza ambaye alifunga mabao 14 msimu uliopita katika Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na Majimaji iliyoshuka daraja, alisema ingawa alizoea kucheza kama kiongozi wa mashambulizi haoni ugumu kucheza pembeni.

Katika mechi zote alizoitumikia Simba kwenye Kombe la Kagame Kaheza alicheza akiwa pembeni kulia na muda mwingi akionekana kuchezesha timu huku akiwatengenezea nafasi za mabao washambuliaji wa kati.

“Hakuna tatizo kucheza winga kwa sababu ni nafasi ambayo pia ninaimudu, nisema kweli kwamba ingawa sijaizoea lakini haijanisumbua nafurahi tu kuaminiwa na kocha na kupata nafasi ya kuanza bila kujali ninacheza wapi unajua Simba ni timu kubwa na hata presha yake ni kubwa tofauti na Majimaji kwa kupata nafasi tu nafurahi na nitajitahidi kuonyesha uwezo wangu,” alisema na kuongeza.

“Ninachoamini nafasi moja ya kucheza kama winga inaweza kuzaa nyingine maana yangu ni kwamba leo naanza kucheza winga lakini kesho inaweza kuwa tofauti,” alisema.

Hata hivyo Kaheza analazimika kupambana kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza ndani ya Simba kwani analazimika kuchuana na Emmanuel Okwi, Mohammed Rashid.

Pia atapata ushindani wa Meddy Kagere, Adam Salamba na nahodha wa timu hiyo John Bocco.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY