Kipre Tcheche kurejea Tanzania katika Timu hii

Kipre Tcheche kurejea Tanzania katika Timu hii

0

Kipre Tcheche kurejea Tanzania katika Timu hii

Unamkumbuka Kipre Herman Tcheche? Nafikiri Unamkumbuka Yule pacha wa John Boco wakiwa pamoja Azam, Pacha iliyokuwa na Uwezo wa Kufunga magoli katika mazingira Yoyote na Kuifanya Azam Fc kuwa na Safu bora ya Ushambuliaji kipindi wakiwa pamoja.

Taarifa za kuaminika ambazo kwataunit.co.ke imezipata ni kwamba Kipre Tcheche anaweza Kurejea nchini katika klabu ya Azam Fc mara baada ya Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa KUFUNGA safari mpaka Malaysia kufanya mazungumzo na timu yake ya sasa Terengganu FC.

Kipre Cheche amebakiza mkataba wa miezi mitatu na  Terengganu FC hivyo Yussuf Bakhresa ameenda Malaysia kufanya nao mazungumzo kwani kuhusu Mchezaji mwenyewe kila kitu wameshakubaliana hivyo timu yake ikikubali basi anatua Azam Fc.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY