Kocha Ndairagije afuata nyayo za Hans Van Pluijm

Kocha Ndairagije afuata nyayo za Hans Van Pluijm

0

Kocha Ndairagije afuata nyayo za Hans Van Pluijm

Kocha wa zamani wa Mbao FC Etienne Ndayiragije, ambaye hivi sasa ni kocha wa KMC ya Kinondoni, ameanza kufuata nyayo za kocha Hans Van Pluijm kwa kuhama na wachezaji wake wa zamani kwenda nao timu mpyan

Mchezaji Sadala Mohamed (katikati) akiwa na viongozi wa klabu ya KMC baada ya kusaini mkataba.

Hatua hiyo imekuja baada ya timu yake ya KMC leo kukamilisha usajili wa mlinzi wa Mbao FC Sadala Mohamed Lipangile. Mlinzi huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia KMC.

Lipangile na kocha Ndayiragije walifanya kazi pamoja kwa takribani msimu mmoja na nusu kwenye klabu ya Mbao FC hivyo bila shaka kocha huyo anatambua uwezo wa mlinzi huyo na ameamua kumuongeza kwenye kikosi chake.

Hans Van Pluijm naye ameungana na nyota wake kadhaa kutoka Singida United kwenda Azam FC ambayo amejiunga nayo kwaajili ya msimu ujao. Nyota hao ni Tafadzwa Kutinyu na Mudathir Yahya ambaye alikuwa Singida United kwa mkopo na sasa amerejea Azam FC na kocha Hans.

KMC ipo kwenye maboresho ya kikosi chake ambapo mbali na mlinzi huyo wa zamani wa Mbao FC pia hivi karibuni imemsajili mlinda mlango mkongwe nchini Juma Kaseja kutoka Kagera Sugar

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY