Kumenoga Jangwani: Usajili Uliokamilika Hadi Sasa Yanga

Kumenoga Jangwani: Usajili Uliokamilika Hadi Sasa Yanga

0
Kumenoga Jangwani: Usajili Uliokamilika Hadi Sasa Yanga.
Ukiachilia mbali kile kinachoitwa usiri mzito wa usajili wa wachezaji kunako klabu ya Yanga, tayari klabu hiyo imekamilisha usajili wa nyota watatu kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.
Kiongozi mmoja  wa klabu hiyo ambaye hakupenda jina lake liwekwe wazi ameuambia mtandao wa kwataunit.co.ke kuwa wachezaji hao ni pamoja na Deus Kaseke ambaye amerejeshwa katika kikosi hicho akitokea Singida United na Mrisho Ngassa na Mcongomani Makambo.
Usajili wa Kaseke amekuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Yanga baada ya Mrisho Ngassa, Mshambuliaji raia wa DRC Congo, Makambo wote wamesaini mikataba ya miaka miwili pia wachezaji hao ndio wameongezwa CAF kwa ajili ya michuano ya kimataifa.
JUMA ABDUL NA KESSY MAMBO FRESH
Wakati Yanga ikitajwa kuwa imeshasajili wachezaji hao kuna Taarifa kuwa walinzi Juma Abdul na Hassan kessy kuwa wameshakaa na Uongozi na mambo yako fresh na Muda wowote wataongeza mkataba wa Kuendelea kuitumikia Yanga.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY