Kwa sifa hizi za Emeka Emerun hakika Yanga imepata mchezaji

Kwa sifa hizi za Emeka Emerun hakika Yanga imepata mchezaji

0

Kwa sifa hizi za Emeka Emerun hakika Yanga imepata mchezaji

Wakati baadhi ya watu wakibeza usajili au baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakitajwa kutua Yanga msimu huu Kamati ya Usajili ya yanga imeendelea kufanya mambo Yake huku ikiendelea kuwatoa hofu wapenzi, washabiki na wanachama wa Yanga kuwa watulie vitu vizuri vinakuja.

Moja ya wachezaji ambao wanatajwa kutua Yanga ni Emeka Emerun Mnigeria aliyekuwa akikipiga nchini Serbia ikiwa amewahi kupita katika klabu kubwa Afrika Esperance na Timu ya Vijana ya Bayern Munich.

Ukiachana kuwa Yanga wamemleta Emeka Emerun kama Mshambuliaji ambaye atakuja Kurithi nafasi za wachezaji kama Donald Ngoma na Obrey Chirwa mchezaji huyo anauwezo wa Kucheza zaidi ya nafasi moja uwanjani.

Emeka Emerun anauwezo wa Kucheza pia kama winga wa Kushoto na Pia winga wa Kulia, lakini pia anaweza kucheza kama mshambuliaji namba 9 na 10 lakini zaidi anauwezo wa kucheza kama kiungo mshambuliaji namba 8 lakini pia akiwa na sifa ya uwezo wa kupiga kwa miguu yote lakini pia mzuri wa Mipira ya Vichwa.

Kama Yanga itafanikiwa kuipata saini Yake basi ni wazi itakuwa imepata mchezaji ambaye anaweza kuwa ni kiraka uwanjani, Mchezaji mmoja mwenye kumudu kucheza nafasi zaidi ya nne uwanjani.

LEO HUENDA AKAONEKANA.

Inaelezwa kuwa Emeka Emerun huenda akaonekana mazoezini uwanja wa Polisi Kurasini Yanga kama mambo yataenda vizuri ili mwalimu Zahera Mwinyi aweze kumuona uwezo wake na Kuruhusu viongozi wamsajili.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY