Maoni ya Peter Manyika kuhusu uwezo wa Rostand

Maoni ya Peter Manyika kuhusu uwezo wa Rostand

0

Maoni ya Peter Manyika kuhusu uwezo wa Rostand

Baada ya lawama nyingi kuonekana kumwangukia kipa wa Yanga Youthe Rostand kutokana na Kuruhusu kufungwa bao 3 katika mchezo kati ya Yanga na Gor Mahia 29 July 2018 Peter Manyika ameibuka na kutoa maoni juu ya uwezo wa Youthe Rostand.

Peter Manyika msomaji wa Kwataunit.co.ke ni kipa wa zamani wa Yanga akicheza kwa mafanikio na Yanga amefunguka na Kutoa maoni tofauti na washabiki wengi ambao wamekuwa wakitupa lawama kwa kipa Huyo.

“Mimi nasema kwanza katika upande wa Yanga kipa aliyesawasawa na kipa anayeibeba Yanga  na kwa hali waliyonayo kwasasa ya Timu ni kipa nayemkubali kwa kila kitu mistake na lawama anazopata ni lawama za Kishabiki “

Aliendelea kwa kusema

” Hata magoli ambayo amekuwa anafungwa ni wazuiaji wanakuwa wanafanya makosa, wanafanya makosa wafungaji wanafunga wakiwa wako Free, Goli nyingi ameokoa na Hata alizofungwa huwezi kumlaumu kikawaida ukiongea kitaalamu “

Peter Manyika aliyekuwa maarufu zaidi uwanjani kutokana na style yake ya kucheza akiwa amevaa kofia uwanjani alisema pia Youthe Rostand licha ya Kufungwa bao zile bado ndiye aliyekuwa man of the match kwa mchezo wa jana kutokana na kuokoa hatari nyingi tena zilizokuwa za hatari zaidi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY