Masoud Djuma akoshwa na uwezo wa mchezaji huyu wa JKU

Masoud Djuma akoshwa na uwezo wa mchezaji huyu wa JKU

0

Masoud Djuma akoshwa na uwezo wa mchezaji huyu wa JKU

Kocha anayeiongoza Simba katika michuano ya Kagame kama kocha mKuu Masoud Djuma jana alishindwa kuficha hisia zake baada ya mchezo kati ya Simba na JKU.

Masoud Djuma baada ya mchezo huo alienda moja kwa moja kwa mchezaji wa JKU Feisal Salum maarufu zaidi kama Fei Toto na kuonekana kumpongeza kwa mchezo mzuri.

Akizungumza baada ya mchezo Masoud alikiri kukoshwa na uwezo wa Fei Toto kutokana na kucheza vizuri eneo la katikati ya uwanja kiasi cha kuwapoteza mara kadhaa viungo wa Simba.

Fei Toto amekuwa pia akitajwa kuwa katika rada za watani wao wa Jadi Yanga ambao wanahaha kuhakikisha wanainasa saini ya Feisal Salum.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY