Matokeo Simba vs JKU Leo 11.7.2018 Kagame

Matokeo Simba vs JKU Leo 11.7.2018 Kagame

0

Matokeo Simba vs JKU Leo 11.7.2018 Kagame

Matokeo Mechi ya Nusu Fainali ya Pili Simba vs JKU Leo 11.7.2018 Kagame Cup 2018 nchini Tanzania, Kwataunit.co.ke Tunakupa Matokeo ya Moja kwa Moja.

Mechi imeanza

Simba 0 – 0 JKU

Dakika ya 2 ya Mchezo bado hakuna Mbabe.

Dakika ya 3 Anaondoka kwa Kasi Mohammed Rashid lakini mpira Unadhibitiwa.

Dakika ya 6 Nassor Juma anawakosa kosa Simba baada ya Kupenyezewa mpira na Feisal Salum “Fei Toto”

Dakika ya 8 Meddie Kagere anapiga Krosi safi Mohammed Rashid anaukosa Mpira Ule, Beki anaupiga nje na Unatoka

Dakika 10

Simba 0 – 0 JKU

Dakika ya 12 Abdulrahman Mussa Wa JKU anawekea pasi ya Upendo lakini anapiga Mpira unapaa

Dakika 15 Feisal Salum “Fei Toto” Anaonekana kuwa msumbufu zaidi eneo la katikati ya uwanja

Simba 0 – 0 JKU

Dakika ya 20 Meddie Kagere kwa mara nyingine anapenyeza mpira lakini Mohammed Rashid anaukosa mpira Ule

Simba 0 – 0 JKU

Dakika 25 Marcel Kaheza anapiga Free kick nzuri inapigwa Kichwa Kipa wa JKU anapangua na Kuwa Kona, Ilikuwa shambulizi zuri kwa Simba

Dakika ya 26 Simba wamechachamaa wanafanya shambulizi jingine zuri kipa Mohammed Abdulrahman anakuwa Shujaa kwa mara Nyingine

Dakika ya 30

Simba 0 – 0 JKU

Dakika ya 36 Pascal Wawa anapanda na anajaribu kupiga Mpira Golini kipa anatoa na kuwa Kona

Dakika ya 41 Simba wanapata Kona

Goaaaaaal Dakika ya 44 Meddie Kagere anaupatia Simba bao, kwa assist ya Nicolas Gyan.

Simba 1 – 0 JKU

HALF TIME

Simba 1 – 0 JKU (41′ Meddie Kagere)

KIPINDI CHA PILI

Dakika ya 50

Simba 1 – 0 JKU (41′ Meddie Kagere)

Dakika ya 57 Meddie Kagere anakosa goli la wazi

Dakika ya 60

Simba 1 – 0 JKU

Dakika ya 63 Mabadiliko kwa Simba anatoka Mzamiru Yassin anaingia Said Hamis Ndemla

Dakika ya 68 Deo Munishi Dida anapiga Chenga kwenye eneo lake almanusra mshambuliaji wa JKU aunase

Dakika ya 69 Pascal Wawa anapanda na Kufanya shambulizi lakini anakosa Mpira

Dakika ya 75, Simba 1 – 0 JKU

Dakika ya 80 Anaingia Rashid Juma anatoka Marcel Bonaventure Kaheza

Dakika ya 82 Rashid Juma anaingia Na Vitu anapiga Krosi safi kwa Kagere ambaye anapia Kichwa Mpira unapaa sentimita chache langoni mwa JKU

Dakika ya 90 Anatoka Mohammed Rashid anaingia Kitandu

Simba 1 – 0 JKU (41′ Kagere)

FULL TIME

Simba 1 – 0 JKU (41′ Kagere)

Fainali ni Azam vs Simba Kagame Cup 2018

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY