Minziro apata timu ya Kuifundisha baada ya Kutoswa KMC

Minziro apata timu ya Kuifundisha baada ya Kutoswa KMC

0

Minziro apata timu ya Kuifundisha baada ya Kutoswa KMC

Siku kadhaa baada ya Kocha aliyeipandisha KMC ligi Kuu kutoka ligi daraja la Kwanza kutoswa kama kocha mkuu wa KMC na nafasi yake kupewa Mburundi Ettiene aliyekuwa Mbao Fc hatimaye Fred Felix “Minziro” amepata Timu.

Fred Minziro amepewa kandarasi ya Kuifundisha Arusha United (JKT Oljoro) kwa muda wa Mwaka mmoja lengo likiwa ni kuipandisha timu hiyo daraja kutoka Lii daraja la kwanza mpaka Ligi Kuu VPL.

Minziro alifanikiwa kuipandisha ligi kuu Singida United msimu wa Mwaka Juzi na msimu wa mwaka jana alifanikiwa kuipandisha ligi Kuu KMC lakini amekuwa akitoswa na timu hizo kama kocha Mkuu baada ya kuzipandisha timu hizo Premier.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY