Mwingine aliyethibitisha Kuongeza Mkataba Yanga

Mwingine aliyethibitisha Kuongeza Mkataba Yanga

0

Mwingine aliyethibitisha Kuongeza Mkataba Yanga

Yanga kila kitu kwasasa kinaonekana Kwenda sawa baada ya awali kuwepo kwa wachezaji wachache tu ambao walikuwa bado wanamikataba huku wengi mikataba ikiwa imeisha.

Wachezaji wengi wa Yanga hata mazoezi walikuwa hawahudhurii kutokana na mikataba yao kuwa Imeisha huku wakisubiri uongozi kuongea Nao.

Wachezaji wengi wameonekana kurejea mazoezini Yanga huku moja ya Wachezaji waliorejea jangwani Geofrey Mwashiuya akithibitisha kuwa ameongeza kandarasi ya miaka miwili kucheza Yanga.

Mwashiuya lakini amefunguka kuwa anatambua hakufanya vizuri msimu uliopita kutokana na kuwa na majeraha ya mara kwa mara ila ameahidi msimu huu kuipambania timu yake na Kuhakikisha Inatwaa mataji mengi timu itakayokuwa Ikishiriki.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY