Pascal Serge Wawa : Wasifu wa Mchezaji (Player Profile)

Pascal Serge Wawa : Wasifu wa Mchezaji (Player Profile)

0

Pascal Serge Wawa : Wasifu wa Mchezaji (Player Profile)

Pascal Serge Wawa ni Mchezaji aliyezaliwa 1 January 1986 Huko Bingerville Nchini Ivory Coast ambayo pia ndiyo Taifa lake la Asili (Raia wa Ivory Coast) akicheza kama Beki wa Kati namba 4 au namba 5 lakini akicheza namba 5 anapokuwa Uwanjani.

Maisha ya Soka ya Pascal Wawa yalianzia  mwaka 2013 katika klabu ya ASEC Mimosas ya nchini Mwake Ivory Coast, Akiwa katika klabu ya ASEC Mimosas Pascal Wawa Alikaa kwenye timu hiyo toka mwaka 2003 mpaka 2010 lakini aliwahi pia Kupata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu ya Fc Lorient ya Ufaransa.

Baada ya Kumalizana na ASEC Mimosas Pascal Wawa mwaka 2010 alijiunga na Klabu ya Al-Merrick ya Nchini Sudan na Kucheza soka lake mpaka mwaka 2014 kwa mafanikio makubwa sana.

Alipotoka katika klabu ya Al-Merrick ya Sudan Pascal Wawa alijiunga na Klabu ya Tanzania Azam Fc ambapo alicheza toka 2014 mpaka mwaka 2016 akiwa moja ya walinzi bora Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara na Kujizolea Umaarufu Mkubwa sana Nchini Tanzania.

Baada ya Kumalizana na Azam Fc 2016  msomaji wa Kwataunit.co.ke Pascal Wawa ALIRUDI Tena nchini Sudan na Kurejea katika klabu yake ya zamani ya Al-Merrick ambapo alicheza mpaka mwaka 2018.

Na Msimu wa 2018/2019 Amesajiliwa na Klabu ya Simba ya Jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania akiwa kama mchezaji huru baada ya Kumalizana na Timu yake ya Al-Merrick.

TIMU YA TAIFA

Amewahi kucheza timu ya Taifa ya Vijana chini ya Miaka 23 mwaka 2008 akicheza jumla ya mechi 4 .

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY