Shabani Idd Chilunda Aondoka Kifalme Azam Fc.

Shabani Idd Chilunda Aondoka Kifalme Azam Fc.

0

Shabani Idd Chilunda Aondoka Kifalme Azam Fc.

Mshambuliaji chipukizi wa klabu ya Azam hapo jana ameiaga klabu yake hiyo kwa kuifungia bao la kwanza kwenye mchezo wa fainali ya Kagame Cup dhidi ya Simba na kumfanya kuondoka klabuni humo akiwa kama mfalme.

Chilunda ambaye ameripotiwa kujiunga na klabu ya Tenerife inayoshiriki ligi ya Segunda division ya nchini uhispania anaondoka Azam baada ya kuiwezesha kutwaa ubingwa wa pili wa mashindano hayo makubwa Afrika Mashariki na Kati huku akiibuka kinara wa upachikaji wa mabao kwa kuifungia timu yake jumla ya mabao 8 kwenye michuano hiyo.

Chilundaambayeatatimiza miaka 20 Julai 20 mwaka huu tangu azaliwe mwaka 1998, alijiunga na akademi ya Azam FC Jumamosi ya Julai 21, mwaka 2012 kabla ya miaka miwili baadaye kupandishwa kikosi cha kwanza.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY