Tetesi za usajili Barani Ulaya 4 July 2018

Tetesi za usajili Barani Ulaya 4 July 2018

0

Tetesi za usajili Barani Ulaya 4 July 2018

Juventus wana uhakika kuwa watamsaimni mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Mchezaji huyo wa umri wa miaka 33 ambaye ni nahodha wa Ureno yuko tayari kukubali mkataba wa pauni milioni 26 kwa mwaka. (Mirror)

Manchester City wako tayari kumsaini wing’a wa Leicester City raia wa Algeria Riyad Mahrez, 27, na kiungo wa kati raia wa Italia Jorginho, 26, kutoka Napoli kwa jumla ya pauni milioni 108. (Mirror)

 

Chelsea wanataka pauni milioni 70 kwa wing’a raia wa Brazil William wakati Barcelona na Manchester United wanamwinda mchezaji huyo wa umri wa miaka 29. (Mundo Deportivo)

Chelsea wamekataa ofa ya zaidi ya puani milioni 50 kwa William kutoka Barcelona. (Sky Sports)

Tottenham wanataka kumsaini kiungo wa kati mfaransa wa umri wa miaka 23 Adrien Rabiot, kutoka Paris St-Germain. (France Football)

 

Meneja wa Arsenal Unai Emery anataka kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona Andre Gomes msimu huu. Mabingwa hao wa Uhispania wanataka pauni milioni 30 kwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ureno. (Independent)

Kiungo wa kati wa Seveilla raia wa Ufaransa Steven N’Zonzi, 29, amekiambia klabu kuwa anataka kuondoka wakati Arsenal inaonyesha nia ya kumsaini. (Sun)

Mshambuliaji wa Chelsea raia wa Uhispania Alvaro Morata, 25, anaweza kutumiwa katika makubaliano ya kubadilishana wachezaji na mshambuliaji raia wa Argentina Gonzalo Higuain 30, kutoka Juventus. (Gazetta dello Sport – in Italian)

 

Derby County wamepewa ruhusa na Chelsea kuzungumzia kuhama kabisa kwa kiungo wa kati wa England Kasey Palmer, 21. (Sky Sports)

Manchester United wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23, wakati Juventus waliacha kumwinda.(Tuttosport via Manchester Evening News)

West Ham wanataka kumchukua mshambuliaji wa Napoli na Italia Roberto Inglese, 26, kwa mkopo. (Il Mattino via Football Italia)

Source : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY