Tetesi za usajili barani ulaya 5 July 2018

Tetesi za usajili barani ulaya 5 July 2018

0

Tetesi za usajili barani ulaya 5 July 2018

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anatathmini ofa kwa kiungo wa kati wa Stoke Xherdan Shaqiri. Mchezaji huyo wa miaka 26 raia wa uswizi anaweza kuondoka Stoke kwa pauni milioni 12. (Sun)

Argentina wanataka meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuwa meneja wao mpya kufuatia kutimuliwa kwao mapema kutoka Komb la Dunia.(AS, via Manchester Evening News)

 

Kiungo mpya wa safu ya kati wa Liverpool Fabinho anasema hakukaribia kujiunga na Manchester United. Mchezaji huyo wa miaka 24 raia wa Brazil alihamia Anfield kutoka Monaco mwezi Mei. (FourFourTwo)

Jack Wilshere amefanya mazungumzo ya ana kwa ana na meneja wa West Ham Manuel Pellegrini kuhusu uwezekano wa kuhamia huko London. Mchezaji huyo wa miaka 26 kiungo wa kati wa England yuko huru baada ya kuondoka Arsenal mwezi uliopita. (Mail)

 

Meneja mpya wa Arsenal Unai Emery anataka kuwauza wachezaji ili kumsaini kiungo wa kati raia wa Ureno Andre Gomes, 24. (Independent)

Manchester City wanamfuatilia kiungo wa kati wa Melbourne City raia wa Australia Daniel Arzani. Mchezaji huo wa miaka 19 alichaguliwa mchezaji bora wa mwaka nchini Australia na anatajwa kuwa Harry Kewell wa siku za usoni. (Manchester Evening News)

Everton wamefanya mawasiliano na Barcelona kuhusu uwezekano wa kuwepo makubaliano kwa mlinzi wa Colombia Yerrt Mina, 23. (Liverpool Echo)

 

Mlinzi wa West Brom raia wa England Craig Dawson, 28, amewasilisha ombi la kutaka ahame baada ya West Brom kukataa ofa kutoka Burnely. (Sky Sports)

Kipa wa West Brom Muingereza Ben Foster, 35, anatarajiwa kukamilisha hatua ya kuhamia Watford kwa pauni milioni 2.5 . (Mirror)

West Ham na Everton wanataka kumsaini mlinzi raia wa Italia Gian Marco Ferrari, 26. (Corriere dello Sport – in Italian)

 

Wing’a wa Newcastle na Scotland Matt Ritchie, 28, amepewa ofa ya mkataba wa pauni milioni 4 kwa mwaka kujiunga na Stoke City. (Sun)

Newcastle wameambiwa kuwa ni lazima wavunje rekodi yao ya kununua wachezaji ikiwa wanataka kumsaini mshambuliaji wa Nice raia wa Ufaransa Alassane Plea, 25, ambaye pia anamezewa mate na West Ham. (Northern Echo)

Hata hivyo Newcastle hawako kwenye mazungumzo kumsaini kiungo wa kati wa Juventus rais wa Italia Stefano Sturaro, 25. (Shields Gazette)

 

Juventus wana uhakika kuwa watamsaini mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 33 ambaye ni nahodha wa Ureno yuko tayari kukubali mkataba wa pauni milioni 26 kwa mwaka. (Mirror)

Manchester City wako tayari kumsaini wing’a wa Leicester City raia wa Algeria Riyad Mahrez, 27, na kiungo wa kati raia wa Italia Jorginho, 26, kutoka Napoli kwa jumla ya pauni milioni 108. (Mirror)

 

Chelsea wanataka pauni milioni 70 kwa wing’a raia wa Brazil William wakati Barcelona na Manchester United wanamwinda mchezaji huyo wa umri wa miaka 29. (Mundo Deportivo)

Chelsea wamekataa ofa ya zaidi ya puani milioni 50 kwa William kutoka Barcelona. (Sky Sports)

Tottenham wanataka kumsaini kiungo wa kati mfaransa wa umri wa miaka 23 Adrien Rabiot, kutoka Paris St-Germain. (France Football)

credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY