Tetesi za usajili barani Ulaya 6 July 2018

Tetesi za usajili barani Ulaya 6 July 2018

0

Tetesi za usajili barani Ulaya 6 July 2018

Masharti ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuhamia katika klabu ya Juventus yalikubaliwa wakati wa mkutano kati ya rais wa Real Florentino Perez , naibu wake Jose Angel Sanchez na ajenti wa Ronaldo Jorge Mendes siku ya Jumatano usiku. (Marca)

Wakati huohuo, Facebook iko katika mazungumzo na Ronaldo kuhusu kipindi cha runinga cha sehemu 13 chenye thamani ya $10m(Variety)

 

West Ham inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere , ambaye yuko huru baada ya kuondoka Arsenal.

Klabu hiyo imempatia kiungo huyo mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya £100,000 kwa wiki (Sun)

Manchester City inakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Itali Jorginho, 26, baada ya Napoli kuthibitisha kuwasili kwa mchezaji atakayechukua mahala pake Fabian Ruiz, 22. (Manchester Evening News)

 

Beki wa Manchester City Aymeric Laporte, 24, anataka kuichezea Uhispania baada ya kuwachwa nje ya kikosi cha Ufaransa katika kikosi cha kombe la dunia (Manchester Evening News)

Manchester United iko tayari kumpatia kiungo wa kati wa Uingereza Jesse Lingard, 25, kandarasi mpya licha ya kuwekai mkataba wa miaka minne mnamo mwezi Aprili. (Sun)

 

Paris St-Germain inataka kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Chelsea N’Golo Kante msimu huu.

Chelsea inataka dau la £100m kwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 lakini pia imemuorodhesha mchezaji wa Lyon mwenye umri wa miaka 21 Tanguy Ndombele, 21, kuchukua mahala pake (Goal)

Tottenham wanapigiwa upatu kumsaini kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 22, lakini mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy anasubiri iwapo klabu hiyo ilioshushwa daraja itakabiliwa na matatizo ya kifedha. (Mirror)

 

Maurizio Sarri anatarajiwa kutangazwa kuchukuwa mahala pake Antonio Conte kama mkufunzi mpya wa Chelsea mwanzo wa wiki ijayo. (Mail)

Klabu mpya iliopandishwa daraja katika ligi ya Uingereza Fulham imejiunga katika mbio za kutaka kumsajili beki wa Celtic na Ubelgiji Dedryck Boyata, 27. (Sun)

 

Everton imekataa ombi la £12m kutoka kwa RB Leipzig kumsaini mshambuliaji wake Ademola Lookman, 20. (Mirror)

Wigan inamtaka kiungo wa kati wa zamani wa klabu ya Sunderland Darron Gibson, 30.

Mchezaji wa huyo wa The Republic of Ireland kwa sasa anafanya mazoezi na the Latics. (Sun)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY