Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 28.7.2018

Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 28.7.2018

0

Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 28.7.2018

Winga wa Chelsea na Brazil Willian, 29, anatarajiwa kujiunga na Manchester United kwa dau la £66m huku klabu hiyo ya Old Trafford pia ikiwa na hamu ya kutaka kumsajili beki wa The Blues mwenye umri wa miaka 32 Gary Cahill. (Express via Tuttosport)

Chelsea imemuorodhesha Kipa wa Uingereza Jordan Pickford, 24, kuwa lengo lao kuu iwapo kipa wake Thibaut Courtois, 26, ataondoka na kuelekea Real Madrid msimu huu (Sky Sports)

Manchester United italazimika kuilipa Leicester dau la rekodi ya £80m kwa Leicester ili kuweza kumleta beki wa Uingereza Harry Maguire , 25, Old Trafford. (Star)

Leicester City inafikiria kuwasilisha ombi la £35m kwa beki wa Newcastle, 24 Jamaal Lascelles, hatua ambayo itamfungulia njia Harry Maguire kuelekea Old Trafford. (Sun)

Manchester United itamuuza Marcos Rojo na Matteo Darmian, 28 ili kupata fedha za kumnunua Maguire. (Mirror)

Wolves inamlenga raia wa Argentine Rojo, 28, huku mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho akianza kuwajaribu mabeki tofauti. (Independent)

Maurizio Sarri yuko tayari kumpatia Eden Hazard cheo cha kuwa nahodha wa Chelsea katika jaribio la kumzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuondoka katika klabu hiyo. (Express)

Chelsea itaendelea kusisitiza dau la kuvunja rekodi la £200m kwa Real Madrid kumnunua Hazard. (Mail)

Crystal Palace inafikiria kumsaini mshambuliaji Danny Ings lakini italazimika kuafikia dau linalohitajika na Liverpool la thamani ya £20m ili kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Guardian)

Leicester City, Newcastle United na Southampton pia wamewasilisha maombi ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Liverpool Ings. (Times – subscription required)

Beki wa Juventus Daniele Rugani amekubali uhamisho wa kuelekea Chelsea lakini ajenti wa mchezaji huyo wa Itali ,23, anasema kuwa klabu hiyo ya Serie A haina haja ya kumuuza. . (London Evening Standard)

Crystal Palace bado ina hamu ya ya kumsaini kungo wa kati wa Senegal Cheikhou Kouyate, 28, huku West Ham ikisubiri maombi ya hadi dau la £10m kwa mchezaji huyo kuuzwa. (Sky Sports)

Chelsea inafikiria kumzuia mshambuliaji wake Alvaro Morata, 25, msimu huu na bado inataka kuwasilisha ombi la kumnunua Gonzalo Higuain, 30 kutoka Juventus. (London Evening Standard)

Besiktas iko katika mazungumzo na Liverpool kuhusu usajili wa kipa wa Ubelgiji Simon Mignolet, 30, huku kiungo wa kati wa Serbia Lazar Markovic, 24, akitarajiwa kuondoka Anfield baada ya kunyatiwa na klabu ya Ugiriki ya Olympiakos. (Mail)

Beki wa kulia wa Arsenal na Uhispania ,23, Hector Bellerin anasema kuwa itakuwa wazimu kuzungumza kuhusu kuondoka katika klabu hiyo licha ya kuhusishwa na uhamisho wa kuelekea Barcelona na Manchester City. (London Evening Standard)

Manchester United imemwambia beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 24, kwamba hauzwi. (Manchester Evening News)

 

Mkufunzi wa Stoke Gary Rowett amepinga uvumi unaomuhusisha kipa wa Uingereza Jack Butland, 25, anayedaiwa kutaka kuelekea Chelsea. (Star)

Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 25, alichapisha ujumbe usioeleweka katika mtandao wa kijamii na kuzua hisia kuhusu hatma yake , huku Everton na Borussia Dortmund zikimnyatia winga huyo mwenye thamani ya £60m . (Mail)

Klabu ya Chelsea ina hamu ya kumsajili Zaha, na inamtaka mchezaji huyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho . (Star)

Aston Villa inafikiria kumsaini kipa wa Ureno,22, Andre Moreira kutoka klabu ya Atletico Madrid, (Sun)

Barcelona itafanya mazungumzo na West ham wikendi hii kuhusu uwezekano wa kumsaini kinda wa The Hammers na Ureno Domingos Quina,18, kwa dau la £600,000 . (Sky Sports)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amemshutumu beki wa Real Madrid Sergio Ramos kwa kuwa na tabia ya mwanamieleka katika ushindi wa Real Madrid wakati wa fainali ya kombe La vilabu bingwa Ulaya.(Guardian)

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY