Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 31.7.2018

Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 31.7.2018

0

Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 31.7.2018

Real Madrid haina mpango wa kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian, mwenye umri wa miaka 29, na wanaemtaka tu ni mlinda lango wa Ubelgiji Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, kutoka the Blues. (marca)

 

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Willian anasema ni mwenye ”furaha sana katika Chelsea na anafurahia kuishi London. (Globo Esporte, via Mirror)

Meneja wa Leicester Claude Puel amesisitizia tena imani yake kwamba mlinzi wa England Harry Maguire mwenye umri wa miaka 25 – anayechezea Manchester United – atasalia na the Foxes katika msimu mpya. (Sky Sports)

Maguire anatarajiwa kupewa donge nono katika mkataba wake mpya na Leicester na hivyo kuongezewa malipo yake ya wiki kutoka £50,000 hadi £95,000. (Mirror)

 

Everton wako mstari wa mbele katika harakati za kusaini mkataba na Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 28 ambae aliambiwa anaweza kuondoka kama tahamani yake ya £30m itatimizwa. (Mirror)

Liverpool wanajiamini kuwa wao ndio watakao saini mkataba na mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, mwenye umri wa miaka 26, kwa mkataba wa muda mrefu mnamo wiki zijazo. (Mirror)

Wakati huo huo , mchezaji wa the Reds kutoka Ubelgiji Divock Origi, 23, anasakwa kwa deni na Besiktas pamoja na Fenerbahce.(Talksport)

The Blues wanaangalia uwezekano wa Kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal kutoka Wales -Aaron Ramsey

Chelsea wamekuwa na mazungumzo ya wazi na Inter Milan juu ya mchezaji wao wa safu ya kati , raia wa Uruguay Matias Vecino, mwenye umri wa miaka 26, na wakatoa £35.5m kwa Juventus ili wamchukue Muitaliano Mattia Caldara mwenye umri wa miaka anayecheza safu ya ulinzi katika timu ya taifa ya Italia. (London Evening Standard)

The Blues pia wanaangalia uwezekano wa Kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal kutoka Wales -Aaron Ramsey, mweney umri wa miaka 27 kwa £30m (Telegraph)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri anasema lengo lake kuu ni kumpata mshambuliaji wa Buyern Munich Robert Lewandowski,

Lazio amembiwa na the Gunners kuwa lazima walipe £7m ikiwa wanataka kusaini mkatapa na mchezaji wa safu ya mashambulizi Muhispania Lucas Perez. (Talksport)

Newcastle wana nia ya kumchukua Nicolas Tagliafico wa Ajax na mchezaji wa kimataifa wa Argentina , lakini gharama ya £8m na madai ya mchezaji huyo wa safu ya nyuma kushoto mwenye umri wa miaka 23 huenda yakawa zaidi ya bajeti iliyopo ya meneja wa Magpies Rafael Benitez. (Newcastle Chronicle)

 

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemtaja mchezaji wa Bayern Munich na mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29, kuwa ndiye mchezaji anayemlenga zaidi kumnunua (Star)

Brighton imekubali kumuuza mshambuliaji wa England Sam Baldock mwenye umri wa miaka 29- kwa Reading. (Argus)

Mourinho amewasihi wachezaji kama Paul Pogba, Romelu Lukaku na Jesse Lingard wapunguze mapumziko yao wawasaidie wachezaji kwenye timu zao wasio na uwezo

Leicester itakubali malipo ya £18m kumnunua mshambuliaji kutoka Algeria Islam Slimani, lakini hatma ya siku zijazo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 haijaamliwa mpaka mwishoni mwa Agosti wakati msimu wa uhamisho utakapomalizi (Leicester Mercury)

Meneja wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amekataa kuingizwa kwenye taarifa za uvumi zinazokihusisha kilabu na uhamisho wa mchezaji wa Chelsea na ttimu ya Ufaransa wa safu ya kati N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 27. (Talksport)

 

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewatolea wito wachezaji kama vile Paul Pogba, Romelu Lukaku na Jesse Lingard, wote wakiwa na umri wa miaka 25, kupunguza mapumziko yao ili kuwasaidia wachezaji katika timu zao wenye uwezo mdogo ambao wameshindwa kufanikiwa kucheza mchezo wa kuridhisha katika kipindi cha kabla ya msimu (Times – subscription required)

Mchezaji wa England anayeichezea kikosi cha Middlesbrough cha vijana walio chini ya miaka 21 kwa sasa Patrick Bamford, mwenye umri wa miaka 24, yuko karibu kuhamia kwa mahasimu wao katika Ligi ya Championi Leeds United kwa gharama ya awali ya awali ya kanda ya £7m. (Guardian)

Wakati huo huo , Boro wamekataa pendekezo la Wolves ambao ni wageni katika Premier League ya kumchukua winga wao Adama Traore mwenye umri wa miaka 22 . (Express & Star)

 

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Morocco Younes Belhanda, anayeichezea Crystal Palace, amemua kuwa hatahamia England na kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 anasisitiza kuwa anafurahia kuwa Galatasary Turkish. (Football.London)

Mchezaji wa safu ya kati wa Paris St-Germain Mfaransa Adrien Rabiot, mwenye umri wa miaka 23, anakaribia kusaini mkataba na Ligue 1 champions. (ESPN)

Mlinzi wa Everton Matty Pennington analengwa na Leeds – ambako alikuwa katika msimu uliopita kwa deni na Wigan pia wanamtaka Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 23.. (Liverpool Echo)

Kocha wa zamani wa walinda lango Kevin Hitchcock ameteuliwa kufanya kazi hiyo hiyo katika timu ya Super Ligi ya India ya Chennaiyin FC -akijiunga na meneja wa zamani wa Aston Villa John Gregory. (Birmingham Mail)

credit : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY