Tetesi za Usajili Simba leo 3 July 2018

Tetesi za Usajili Simba leo 3 July 2018

0

Tetesi za Usajili Simba leo 3 July 2018

Simba ni moja ya Vilabu ambavyo usajili wake umekuwa wazi huku mpaka sasa wakianza kula matunda ya Usajili wake katika michuano ya Kagame Cup kwa washambuliaji waliosajiliwa kuanza vyema kwa Kufunga na Mabeki kama Wawa kuwa Visiki kweli kweli.

Ulisikia taarifa za Simba kuhitaji huduma ya Kiungo wa Mtibwa Sugar Hassan Dilunga, sasa ishu hiyo unaambiwa Simba wameshaongea na Dilunga na Mchezaji huyo amekubali ila kinachokwamisha ni boss wa Mtibwa Sugar Jamal Byser.

Inaelezwa kuwa Byser amekuwa na Ofa Mbili ya Hassan Dilunga moja kutoka Difaa El Jadid na Moja kutoka Simba lakini Taarifa zaidi msomaji wa Kwataunit.co.ke zinasema kuwa Difaa wamekuwa Kimya kiasi tofauti na Simba ambao wameonyesha mahitaji makubwa hivyo huenda Simba wakawa kwenye nafasi kubwa zaidi ya Kumsajili.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY