Tetesi za usajili Yanga leo 10 July 2018

Tetesi za usajili Yanga leo 10 July 2018

0

Tetesi za usajili Yanga leo 10 July 2018

BEKI wa kulia wa Gor Mahia ya Kenya, Mrundi, Karim NIzigiyimana, amefunguka kuwa yupo tayari kujiunga na Yanga kwa ajili ya msimu ujao kutokana na mkataba wake na timu hiyo kuelekea ukingoni huku akisisitiza ni ndoto yake ya muda mrefu kucheza kwenye ligi ya Bongo kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

Nzigiyimana ambaye anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kushambulia pamoja na kupiga krosi za maana, amesema licha ya kukaa nje muda mrefu akiwa anauguza majeraha ya goti aliyoyapata kwenye ligi ya Kenya, anaamini kwa sasa ni wakati wake kujiunga na Yanga ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu.

 

Akizungumza nasi beki huyo alisema kuwa moja ya ndoto zake kubwa ni kuona anacheza ligi ya Tanzania huku akiamini Yanga ni sehemu sahihi kutokana na ushindani uliopo.

 

“Nilishapona na mazoezi nimeanza na ilibidi nije katika mashindano ya Kagame lakini nimeona niendelee kujifua ili nirudishe kiwango changu cha awali. Natamani kuja Yanga.

“Nimesikia hawapo vizuri lakini kwangu hiyo siyo tatizo kama watakuja tuzungumze kwa sababu ndoto yangu ni kuona nacheza ligi ya Tanzania ambayo imekuwa na ushindani mkubwa na ukiangalia Yanga kwa jinsi ilivyo naamini nitakuwa msaada kwao,” alisema Nzigiyimana.

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY