Tetesi za Usajili Yanga leo 6 July 2018

Tetesi za Usajili Yanga leo 6 July 2018

0

Tetesi za Usajili Yanga leo 6 July 2018

Baada ya kuelezwa kuwa Yanga imeshamalizana na wachezaji kadhaa wakiwemo Mrisho Ngassa ” Anko ” , Jaffar Mohammed wa Maji Maji, Heritier Makambo na Mnigeria Emeka Emerun kuna Mcongo mwingine huenda akatua Yanga.

Taarifa za Uhakika ambazo kwataunit.co.ke imezipata Kutoka kwenye chanzo cha Kuaminika inaelezwa Yanga wapo katika mazungumzo na Mchezaji wa zamani wa  Dc Motema Pembe Yannick Bangala Litombo ambaye inaelezwa kwasasa alikuwa As Vita ya Huko huko Congo na Mkataba wake umeisha 30 June 2018.

SIFA ZAKE.

Yannick Litombo Ni mchezaji mwenye Umri wa Miaka 24 akizaliwa 12 April 1994 akicheza katika vilabu kama Fc Les Stars, Motema Pembe na As Vita ambayo mkataba wake umemalizika.

Yannick Litombo Anauwezo wa Kucheza kama beki wa Kati lakini pia kiungo wa Ukabaki akianza kucheza pia timu za Taifa za Vijana za Congo kama ile ya chini ya Miaka 20 na ya Wakubwa ya Congo mara kadhaa akiwa kama Nahodha pia wa Timu ya Taifa ya Congo.

Anapokuwa Uwanjani anauwezo mkubwa wa Kukaba, Kucheza mipira ya Juu (Mipira ya Kichwa)  lakini pia ni mzuri kwenye kuanzisha mashambulizi anapocheza uwanjani kutokana na uwezo wa Kupiga mipira mirefu na Pasi za Uhakika.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY