Thomas Ulimwengu azidi kucheka na Nyavu Sudan

Thomas Ulimwengu azidi kucheka na Nyavu Sudan

0

Thomas Ulimwengu azidi kucheka na Nyavu Sudan

Mshambuliaji Nyota wa Tanzania anayecheza soka la Kulipwa nchini Sudan Thomas Ulimwengu amezidi kucheka na Nyavu akiwa na Klabu yake ya Al Hilal ya inayoshiriki ligi kuu ya Sudan.

Thomas Ulimwengu siku ya jana aliweza kufunga bao moja wakati timu yake ikipata ushindi wa Bao 4 kwa 0 dhidi ya Hay Al arab mchezo wa Ligi ya Sudan.

Hii inakuja ikiwa ni siku kadhaa toka Thomas Ulimwengu aifungie timu yake bao katika Mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF.

Lakini kabla ya mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Thomas Ulimwengu July 8 mwaka huu aliifungia timu yake bao 2 ikipata ushindi wa bao 4 ikiwa ndiyo mechi yake ya Kwanza ya Ligi na Al Hilal.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY