Timu 11 VPL ambazo hazijafanya usajili kwenye Mfumo wa Usajili

Timu 11 VPL ambazo hazijafanya usajili kwenye Mfumo wa Usajili

0

Timu 11 VPL ambazo hazijafanya usajili kwenye Mfumo wa Usajili

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linavikumbusha vilabu vya Ligi Kuu,Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ambavyo havijafanya usajili kupitia mfumo wa usajili wa TFF FIFA Connect kufanya usajili wao.
Vilabu ambavyo bado havijafanya usajili wawasiliane na TFF kama kuna msaada wowote wanahitaji ili kukamilisha usajili wao.
Dirisha la Usajili litafungwa Alhamis Julai 26,2018 na TFF inasisitiza hakutakuwa na muda wa ziada katika usajili.
Timu ambayo itashindwa kukamilisha usajili haitaruhusiwa kushiriki Ligi ya msimu ujao wa 2018/2019.
Vilabu ambavyo havijafanya usajili mpaka sasa
LIGI KUU:
Ruvu Shooting,Mbeya City,Tanzania Prisons,Mtibwa Sugar,Mwadui,Kagera Sugar,Alliance,Lipuli,African Lyon,KMC na Azam

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY