Ufaransa Mabingwa  Kombe La Dunia 2018

Ufaransa Mabingwa  Kombe La Dunia 2018

0

Ufaransa Mabingwa  Kombe La Dunia 2018

Timu ya Ufaransa ni mabingwa wa finali za kombe la dunia 2018 baada ya kuwafunga Croatia kwa magoli manne kwa mbili (4-2).

Kocha Didie Deschamps amekuwa mtu wa tatu kushinda kombe la dunia akiwa mchezaji na kocha wengine ni Mario Zagallo na Franz Beckenbauer

Mario Mandzukic amekuwa mchezaji wa 5 kufunga katika fainali za kombe la dunia na Uefa Champions league wengine nu Ferenc Puskas, Zoltan Czibor, Gerd Muller na Zinedine Zidane.

Mario Mandzukic amekuwa mchezaji wa kwanza kujifunga goli katika fainali ya kombe la dunia.

Kylian Mbappe amekuwa mchezaji wa pili kinda kufunga goli katika fainali ya kombe za dunia, Mbappe ana miaka 19 na siku 207 anayeongoza ni Pele alifunga katika fainali za mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 17 na siku 249

Paul Pogba amekuwa mchezaji wa kwanza kuifungia Ufaransa goli katika fainali ya kombe la dunia kutoka Premier league mara ya mwisho mchezaji kutoka Premier league kuifungia goli Ufaransa katika fainali alikuwa Petit katika fainali za mwaka 1998

Ivan Perisic amehusika katika magoli mengi zaidi ya mchezaji yoyote wa Croatia amehusika katika magoli 11 (7 goals, 4 assist) ya Croatia katika mashindano makubwa.

FT Ufaransa 4-2 Croatia
18′ Mandzukic (og) 28′ Perisic
38′ Griezmann (p) 69′ Mandzukic
59′ Pogba
65′ Mbappe

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY