Ujumbe Wa Manara Kwa Mashabiki Kuelekea Mechi Ya Leo Dhidi Ya Azam.

Ujumbe Wa Manara Kwa Mashabiki Kuelekea Mechi Ya Leo Dhidi Ya Azam.

0

Ujumbe Wa Manara Kwa Mashabiki Kuelekea Mechi Ya Leo Dhidi Ya Azam.

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amewataka wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo leo itakaposhuka dimbani katika mchexo wa fainali dhidi ya Azam fc.

Kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 12:00 jioni kwenye uwanja wa taifa Simba itwmakuwa na kibarua kizito kuwakabili mabingwa watetezi wa kombe hilo linalojumuisha vilabu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika mashariki na kati.

Katika ujumbe alioandika Manara kwenye ukurasa wake wa instagram ameandika,“Le grand spokesman anawaomba sana Wanasimba tuje kwa wingi Taifa leo kuishangilia timu yao.’ Tunaiheshimu Azam fc na tunajua ubora wao but We are big club na tunajua nn maana ya fainali..Inshaalla We will make it..

Jumaa Maqboul”

Kabla ya mchezo huo kutakuwa na mtanange wa kumsaka mshindi wa tatu ambao utapigwa majira ya saa 9:00 alasiri na kuzikutanisha timu za JKU ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY