USAJILI Uliokamilika VPL katoka Simba kwenda Mtibwa

USAJILI Uliokamilika VPL katoka Simba kwenda Mtibwa

0

USAJILI Uliokamilika VPL katoka Simba kwenda Mtibwa

Mabingwa wa kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup) Mtibwa Sugar Sports Club, leo wamefanikisha kuinasa saini ya Juma Luizio.

Luizio aliyekuzwa na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar na baadae kutimkia Zambia kucheza soka la kulipwa na msimu huu amesajiliwa na Mtibwa Sugar akitokea Simba Sc ya jijini Dar es salaam.

Usajili wa Juma Luizio kwa wana tam tam ni saini ya pili kwa mabingwa hao wa kombe la Azam Sports Federation Cup baada ya kufanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji mwingine Jaffary Salum Kibaya kutoka Kagera Sugar ambaye pia alikuzwa na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar kabla ya kutimkia Kagera Sugar msimu jana.

“usajili wa Luizio ni mapendekezo ya benchi la ufundi  na kikosi chetu hakitakuwa na mabadiliko makubwa sana hivyo tutarajie kuziona sura zile zile za msimu jana”Abubakar Swabr

Aidha kikosi cha Mtibwa Sugar kimeendelea na mazoezi yake jijini Dar es salaam chini ya  makocha wake Zuber Katwila na Patrick Mwangata wakishirikiana na mkurugenzi wa ufundi Salum Mayanga

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY