USAJILI : Waliosajiliwa na Kutoka dakika za Mwisho VPL

USAJILI : Waliosajiliwa na Kutoka dakika za Mwisho VPL

0

USAJILI : Waliosajiliwa na Kutoka dakika za Mwisho VPL

Wakati Dirisha la Usajili likiwa limefungwa rasmi siku ya Jana majira ya saa 6 Usiku wapo wachezaji usajili wao ulikamilika siku ya Jana ikiwa ndiyo siku ya Mwisho kabisa ya usajili.

Simba

Simba wao walifanikiwa kumbakiza nyota wake Said Ndemla ambaye alikuwa akihusishwa kutua Yanga kwa Muda mrefu lakini pia katika klabu moja huko nchini Sweden kabla ya dili zote kukwama na Kuamua kuongeza mkataba wa miaka 2 Simba.

Yanga

Yanga wao wamekamilisha usajili wa Nyota wao wawili kutoka Congo kipa Nkizi Kindoki na Mshambuliaji Heritier Makambo huku beki Kitasa Kelvin Yondani naye akisaini rasmi Yanga miaka 2.

Naye Kipa Beno Kakolanya naye amefanikiwa kuongeza mkataba wa Miaka miwili kuendelea kucheza soka katika klabu ya Yanga

Yanga washindwa kumbakiza nyota wake Huyu aliyeamua kutosaini Yanga.

Yanga wameshindwa Kumjumuisha Hassan Kessy ambaye yeye anatajwa Kutua Nkana Fc ya nchini Zambia.

Azam Fc na Singida United

Timu ya Azam Fc imefanikiwa kumnasa Danny Lyanga kwa kandarasi ya Mwaka mmoja huku Singida wao wakimnasa Geof Mwashiuya kutoka Yanga akisaini miaka miwili na mshambuliaji mwingine Mghana, Hans Kwofie akitokea Smouha S.C ya Misri ambaye naye amesaini miaka miwili.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY