USAJILI: Yanga sasa Kumnasa Straika aliyemkalisha Kagere Kenya

USAJILI: Yanga sasa Kumnasa Straika aliyemkalisha Kagere Kenya

0

USAJILI: Yanga sasa Kumnasa Straika aliyemkalisha Kagere Kenya

Wakati washabiki wa Yanga wakiwa wameanza kuwa na Furaha kiasi mara baada ya Uongozi wa Timu yao kuanza kutangaza silaha moja moja waliyoinasa kwaajili ya Vita Ijayo

Inaelezwa kuwa Tayari Yanga imeanza harakati za Kuitafuta Straika ambaye ndiye anayeongoza kwa magoli nchini kenya kwa sasa akimfunika mpaka Straika wa sasa wa Simba Meddie Kagere.

Straika huyo wala hata hachezi vilabu vikubwa nchini Kenya akicheza katika klabu ya Nzoia Sugar Rupia, Elvis Baranga ambaye timu yake ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa timu 18 lakini bado anaongoza kwa Magoli.

Straika huyo anajumla ya Magoli 15 mpaka sasa katika Mechi 22 ambazo timu yake Imecheza huku Meddie Kagere mpaka anaondoka akiwa na Magoli 8 pekee na hata wakati anaondoka na Mabao yake 8 Elvis Baranga alikuwa na Magoli hayo 15.

UTATA ULIPO.

Licha ya Kuwa Yanga wanaweza kuipata saini ya Straika huyo kulingana na mchezaji wao wa zamani na kocha wa zamani wa Nzoia Sugar na mchezaji huyo Ben Mwalala inaelezwa kuwa bado anamkataba wa mwaka mmoja na Nzoia hivyo itawabidi Yanga wavunje mkataba ili kumsajili kitu ambacho inaelezwa Yanga wapo tayari.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY