Wachezaji wa Simba ambao hawataondoka na Kikosi kwenda Uturuki

Wachezaji wa Simba ambao hawataondoka na Kikosi kwenda Uturuki

0

Wachezaji wa Simba ambao hawataondoka na Kikosi kwenda Uturuki

Kikosi cha Simba SC kimeondoka leo alfajiri kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara.

Kikosi hicho kitarejea nchini August 05 kwa ajili ya Tamasha lao maalumu la kila mwaka ‘ Simba Day’ ambalo hufanyika kila ifikapo tarehe 08 August ya mwaka.

Simba jana waliwatanguliza watu 5 wa bechi la ufundi ambao ni Kocha Msaidizi wa klabu hiyo Masoud Djuma, Kocha wa makipa Mwalmi Mohammed, Daktari wa timu Yassin Gembe, Meneja wa Richart Robart na mtunza vifaa wa klabu hiyo.

Baadhi ya wachezaji wameachwa kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili na wengine wataungana na timu baadae akiwemo kiungo Said Ndemla ambaye ameachwa kwa sababu ya kushungulikia mkataba mpya na klabu hiyo,mkataba wake wa awali na Simba unaisha juma lijalo na bado hajasaini mkataba mpya mpaka sasa. Erasto Nyoni amechwa kwa sababu ya matatizo ya kifamilia na anatarajiwa kuungana na wenzake kambini Uturuki jumatano ijayo.

  • Magazeti Ya michezo leo 22.7.2018

    Pia magolikipa Emanuel Mseja na Said Mohamed Nduda wameachwa kwa ajili ya kutolewa kwa mkopo kabla dirisha la Usajili halijafungwa siku sita zijazo.

Credit : Samuel Samuel

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY