Wachezaji Yanga waliogoma kutokea Mazoezini mpaka sasa

Wachezaji Yanga waliogoma kutokea Mazoezini mpaka sasa

0

Wachezaji Yanga waliogoma kutokea Mazoezini mpaka sasa

Wakati Yanga ikiwa imekamilisha usajili wa Wachezaji wanne na Kuwatangaza mbele ya Waandishi wa Habari ambao ni Feisal Salum “Fei Toto” , Jaffar Mohammed, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke bado kazi wanayo kwa wachezaji waliomaliza Mikataba.

Wakati juzi kati wachezaji wengi wakiripotiwa kutokea Mazoezini baada ya kutoonekana kwa muda kiasi wachezaji Kelvin Yondani na Hassan Kessy ndiyo bado hawajaonekana mazoezini mpaka sasa.

Wengine kama Beno Kakolanya, Juma Abdul na Andrew Vincent walitokea Mazoezini siku kadhaa kabla ya jana nao kuripotiwa Kukacha mazoezi kwa Kutotokea Huku sababu zikielezwa ni kutotimiziwa baadhi ya Mahitaji yao ikiwa ni pamoja na kusaini mikataba mipya.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY