Walichosema mtibwa baada ya tetesi za Hassan Dilunga Kutua Simba

Walichosema mtibwa baada ya tetesi za Hassan Dilunga Kutua Simba

0

Walichosema mtibwa baada ya tetesi za Hassan Dilunga Kutua Simba

Wakati kukiwa na Tetesi nyingi zinazotajwa kumhusu Kiungo wa Mtibwa Sugar Hassan Dilunga kutajwa kuwa katika Rada za Usajili wa Mabingwa wa Soka Nchini Tanzania Bara Simba , Mtibwa wenyewe wameibuka na Kutoa Kauli Yao.

Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar Jamal Byser amefunguka na Kusema kuwa Hakuna chochote kinachoendelea kati ya Simba na Wao kumhusu Hassan Dilunga.

Jamal Byser amesema Hassan Dilunga ambaye pia amewahi kucheza Yanga bado anamkataba wa Mwaka mmoja wa kucheza Mtibwa Sugar na wao kama Mtibwa wanaamini ataendelea Kucheza Mtibwa.

“Taarifa hizo kweli zinazungumzwa sana lakini suala la Dilunga Kujiunga Simba halipo, Nafikiri ni tetesi na wakati wa Usajili tetesi huwa zinakuwa nyingi, Dilunga bado anamkataba wa Mwaka mmoja na nafikiri bado ataendelea kuitumikia Mtibwa Sugar “

Jamal Byser amefunguka pia wameshafanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji kwaajili ya Usajili lakini bado mambo hayajakamilika na Mchezaji pekee waliyemsajili ni Jaffary Kibaya.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY