Yanga wasajili mchezaji aliyesaini Singida kisha akazungumza na Simba

Yanga wasajili mchezaji aliyesaini Singida kisha akazungumza na Simba

0

Yanga wasajili mchezaji aliyesaini Singida kisha akazungumza na Simba

Baada tu ya mchezo wa jana kati ya JKU na Simba, vigogo wa Simba walianza mchakato wa kumalizana na kiungo wa JKU, Feisal Salum Abdallah (Fei Toto).

Taarifa za ndani zinadai hadi saa 7 usiku walikuwanae na wakakubaliana dau la sh. 50 mil huku Wekundu hao wakiwa tayari kuilipa Singida United sh. 18 mil walizompa kinda huyo baada ya kusaini mkataba wa awali wa sh. 28mil.

Baada ya Mohammed Issa Banka inatajwa kuwa huenda Yanga wakamtangaza na mchezaji  Huyu

Kikao hicho kilichohusisha pia viongozi wa JKU kilimalizika kwa makubaliano leo saa 4 asubuhi Simba waingize ‘mzigo’ benki biashara ikamilike. Wakati hayo yakiendelea Singida waliamua kuziachia picha na video zilizochukuliwa miezi miwili iliyopita wakati wanamsainisha

Picha zinazoaminika zilipigwa miezi miwili iliyopita.

lakini hiyo haikutosha kuwazuia Yanga kuingilia kati na kumteka ‘Dogo’ huyo Mtandao huu unafahamu hadi sasa wapo nae maeneo ya Temeke huku wakiendelea na majadiliano na upande wa Singida ili wakubali kurejeshewa pesa yao Feisal amwage wino Jangwani.

Ambapo kuna Taarifa za Uhakika kuwa tayari ameshamwaga wino kucheza Yanga kwaajili ya msimu Ujao.

Source : Boiplus

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY