Zamalek yamnasa kocha wa Tottenham Hotspur

Zamalek yamnasa kocha wa Tottenham Hotspur

0

Zamalek yamnasa kocha wa Tottenham Hotspur

Klabu ya Zamalek ya nchini Misri Imemtangaza kocha wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspur na klabu ya Basel Christian Gross kama kocha wao mpya.

Tetesi za Christian Gross kutua Zamalek zilianza toka mwezi wa nne mwaka huu na Baadaye kuyeyuka lakini Jana Christian Gross ametangazwa rasmi kuwa kocha wa Zamalek.

Christian Gross amesaini kandarasi ya Mwaka mmoja na mabingwa hao wa zamani wa Misri na Afrika akichukua nafasi ya kocha aliyekuwa wa muda Khaled Galal.

Baada ya Kutambulishwa Kocha Christian Gross ameshukuru uongozi wa Zamalek kwa Kumuamini, Kabla ya Kujiunga na Zamalek kocha huyo alikuwa akifundisha Al-Ahli ya Saudi Arabia.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY