Arusha United vs Simba leo 15.8.2018

Arusha United vs Simba leo 15.8.2018

0

Arusha United vs Simba leo 15.8.2018

Timu mbalimbali za Ligi kuu soka ya Tanzania Bara zinaendelea na amandalizi ya Ligi kuu soka ya Tanzania Bara msimu wa 2018/2019 huku baadhi ya timu zikicheza michezo ya Kirafiki.

Baada ya kucheza na Namungo Fc jumamosi ya wiki iliyopita Agosti 11, 2018 huko wilayani Ruangwa klabu ya Simba leo inashuka tena dimbani kucheza mchezo mwingine wa Kirafiki.

Simba itacheza na klabu ya Arusha United (Zamani JKT Oljoro) katika uwanja wa Sheikh Amri Abeib jijini Arusha mechi itakayoanza majira ya saa kumi kamili jioni.

Kuelekea mechi hiyo timu zote zimetambiana huku afisa habari wa Simba Haji manara akiahidi kujiuzulu endapo tu Simba itafungwa na Arusha United.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY