Baada ya Kocha Mkongo kusepa huyu hapa anatajwa kutua Yanga

Baada ya Kocha Mkongo kusepa huyu hapa anatajwa kutua Yanga

0

Baada ya Kocha Mkongo kusepa huyu hapa anatajwa kutua Yanga

Asikwambie Mtu Yanga wanaendelea kupambana na hali zao lakini katika hali ya Umakini na Kuhakikisha hawakosei kwenye kila step wanayofanya hasa katika masuala ya kiufundi.

Yanga katika suala la timu yao hawajataka kukwama na wanaakikisha wanajitoa mpaka kwenye kiwango chao cha Mwisho na ndiyo maana walifaulu kuwabakiza nyota wake muhimu ambao walimaliza mikataba lakini pia kunasa saini za baadhi ya nyota muhimu ili kuimarisha Kikosi chao.

Baada ya Kocha Mkongo Gay Bukasa alliyekuja kama msaidizi wa Zahera kuondoka Kimya Kimya Inaelezwa Yanga wameanza kutafuta kocha msaidizi Mzawa ili kuimarisha benchi la Ufundi.

Kwa upande wa Benchi la Ufundi Yanga ianelezwa kuwa katika mipango ya kuzidi kuboresha kikosi chao kwa kuleta kocha wa Makipa na Kocha mwingine msaidizi ambaye atakuwa mzawa kuchukua nafasi ya Kocha Shadrack Nsajigwa ambaye mkataba wake na Yanga ulipomalizika hakuongezewa tena.

Upande wa Kocha wa Makipa tayari inaelezwa kuwa Juma Pondamali huenda akatemwa katika nafasi hiyo na mkenya Razack Siwa alishatua nchini na Kufanya mazungumzo na Viongozi wa Yanga kabla ya Kocha huyo kurejea kwao nchini Kenya

Katika kuhakikisha Yanga inakuwa vyema kwenye upande wa Benchi la ufundi inaelezwa kuwa Yanga wapo katika mipango mathubuti ya Kunasa saini ya Aliyekuwa kocha wa Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na mchezaji na Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Meck Mexime.

Inaelezwa Yanga walianza kumfukuzia Mexime mapema lakini kwasasa wanaona ni wazi wanahitaji zaidi huduma Yake ili aweze kuwasaidia katika kipindi hiki.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY