Baada ya kuhusishwa kurejea Yanga Haruna Niyonzima afunguka haya

Baada ya kuhusishwa kurejea Yanga Haruna Niyonzima afunguka haya

0

Baada ya kuhusishwa kurejea Yanga Haruna Niyonzima afunguka haya

Katika vitu ambavyo vimekuwa gumzo kwa wapenzi na washabiki wa SImba ni juu ya Hatma ya mchezaji wao Haruna Niyonzima ndani ya klabu hiyo.

Hii inakuja kutokana na kuwepo kwa Sintofahamu juu ya hatma yake ndani ya klabu, Kutokwenda kwenye kambi ya Uturuki lakini pia kutotambulishwa kwa mchezaji huyo siku ya Simba “Simba Day”

Kutokana na HAYO yote kumekuwa na maswali mengi juu ya nini kitafuata kwa Uongozi wa Simba na Haruna Niyonzima

Kuna taarifa zilisemekana kuwa Huenda mchezaji  huyo akarejea Yanga klabu yake ya zamani kutokana na uongozi wa Simba kuona Niyonzima anawazingua lakini hali hiyo ikizidi kunogeshwa na uwezo wa Cletous Chama ambaye anacheza nafasi sawa na Niyonzima.

Lakini kiungo huyo Kutoka nchi ya Rwanda ambaye amewahi kucheza Yanga kwa mafanikio makubwa kabla ya kusajiliwa na Simba msimu uliopita amefunguka kuwa yeye bado anamkataba na Simba na hakuna timu inayomhitaji

Na tatizo pekee lililokuwepo kati yake (Haruna Niyonzima ) na Simba ni kuchelewa kuripoti kambini na tayari wameshazungumza na Uongozi lakini aligoma kusema walichozungumza na maamuzi yaliyofikiwa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY