Baada ya Kusikia kiwango hiki cha pesa MAKAMBO ahaidi kuwafunga Waarabu

Baada ya Kusikia kiwango hiki cha pesa MAKAMBO ahaidi kuwafunga Waarabu

0

Baada ya Kusikia kiwango hiki cha pesa MAKAMBO ahaidi kuwafunga Waarabu

Kama ulifikiri Yanga wamekata tamaa na michuano ya Kimataifa basi utakuwa unafeli asubuhi tu kabla hata ya jua kuchomoza.

Licha ya kuwa ni ukweli Yanga hawana nafasi ya kufuzu hatua inayofuata kombe la Shirikisho barani Afrika kutokana na Idadi ya Points walizonazo.

Lakini unaambiwa wao akili imeamia kwenye kuhakikisha wanapata nafasi ya Tatu kwa namna yoyote ile inayowezekana.

Moja ya watu waliofunguka kuhusu ishu hiyo ni Straika raia wa Congo Makambo Heritier ambaye baada ya kusikia kuwa Yanga wakiwa nafasi ya tatu na ya nne mkwanja ni tofauti.

Bonyeza hapa KULike Ukurasa wetu wa facebook kuzipata habari kwa Haraka zaidi

ISHU IKO HIVI

Heritier Makambo baada ya kujua kuwa timu inayoshika nafasi ya tatu inakula mkwanja mrefu zaidi ya timu inayokuwa ya Nne amefunguka kuwa atahakikisha Yanga inapata ushindi kwenye mchezo huo kwa kutumia vizuri nafasi zote ambazo Yanga itazipata.

Yanga ikishika nafasi ya nne itakusanya kiasi cha Milioni 340 hivi za Kitanzania wakati ikiwa nafas ya tatu kwenye kundi itakusanya zaidi ya milioni 500 za Kitanzania.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY