Baada ya Simba vs Asante Kotoko Kocha Yanga ataja wachezaji 2 hatari...

Baada ya Simba vs Asante Kotoko Kocha Yanga ataja wachezaji 2 hatari Simba

0

Baada ya Simba vs Asante Kotoko Kocha Yanga ataja wachezaji 2 hatari Simba

Kama unafikiri kocha wa Yanga hawafatilii Simba basi utakuwa unajidanganya kwani kocha Huyo siku ya Jumatano 8.8.2018 alikaa kwenye Tv na Kucheki pambano kati ya Simba na Asante Kotoko kutoka Ghana.

Kocha Mwinyi Zahera ambaye ndiye kocha mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa Baada ya Kuangalia pambano hilo amewaona wachezaji hatari wawili kwenye kikosi cha Simba.

Wachezaji hao ni Emmanuel Okwi ambaye amesema licha ya Kuwa mchezaji huyo hakuwa na Ari ya mchezo lakini bado alionyesha anavitu vingi na hakukata tamaa mpaka akafanikiwa kufunga bao.

Mchezaji mwingine ambaye Mwinyi Zahera anakiri kuwa Simba imepata mchezaji mzuri msomaji wa kwataunit.co.ke  ni Cletous Chota Chama ambaye anacheza nafasi ya Kiungo.

Mwinyi Zahera amefunguka kuwa Chama ni mchezaji mzuri sana na alishudia akipiga pasi nzuri za mwisho zaidi ya 9 ambazo washambuliaji wangekuwa makini basi Simba ingeshinda nyingi lakini pia amesifu aina yake ya Upigaji pasi kwani anauwezo wa Kupiga pasi za Kila aina.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY