Baada ya washabiki kusema Kocha Hafai Manara aandika Ujumbe Huu

Baada ya washabiki kusema Kocha Hafai Manara aandika Ujumbe Huu

0

Baada ya washabiki kusema Kocha Hafai Manara aandika Ujumbe Huu

Wakati baadhi ya washabiki wa Simba wakiwa wanafurahia ushindi dhidi ya Tanzania Prisons ushindi wa bao 1 kwa 0, Baadhi ya washabiki wamechukizwa na kiwango na ushindi huo kiduchu.

Afisa habari wa Simba ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe kwenda kwa washabiki wanaoponda ushindi huo na baadhi kwenda mbali kwa kusema kocha hafai.

Ujumbe wa Haji Manara.

Salaam 
wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!!
Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons!!
Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kama hesabu..hisabati 3×3 ni tisa tu..hata ukokotoe vipi! Huku kwetu kwenye ndiki 3×3 inaweza kuwa bilioni nane 
Mara nyingi huwa nakataa kuwepo kwenye groups za WhatsApp sababu asilimia kubwa mpira wameujulia mitandaoni..hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa!!
Kwao hudhani kila siku Simba itashinda na kwao ushindi ni lazma upate goli saba au tano..kwao ushindi ni mnono tu..hata kama unakutana na Wanaume wenzako!
Wanabeza huku wakisahau Prisons iliingia top four Msimu uliopita,wanabeza huku wakijua Prisons haifungwi kitoto kama Mnyela United!
Halaf wanakuja na hoja dhaifu inayopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja? Afana aleik!!
Hapo ndio Haji naonekana mtata..aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulienda camp ya pre season.ni mazoezi ya mwanzo wa msimu
Wengine walienda Zanzibar kama Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba..kote huko ilikuwa inatafutwa chemistry ya team toka kwa makocha.
Ni lazma mnapoamua kuushabikia mchezo huu mjifunze sayansi yake na msijifunze sayansi hii kiwepesi wepesi kama mnajifunza Sayansi kimu 
Leo tumecheza na team nzuri na walijiandaa kama tulivyojiandaa cc..na lazma muelewe mfumo wa kocha hauingii kwa kipindi kifupi..unachukua muda kdogo..
Niwasihi sana Wanasimba Soka ni zaidi ya mchezo wa draft au Chess ya kina kasparov na karpov..inahitaji shabiki kabla ya kulaumu ajue vtu vingi kdogo kwenye medula yake..vinginevyo ni kufanya uchale tu 
Sina maana tunakataa ushauri ila uwe ushauri unaoendana na taaluma na kama huna jijengee busara ya kupiga kimya..usifate mkumbo wa mitandaoni

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY