Barcelona Mabingwa Super Cup 2018

Barcelona Mabingwa Super Cup 2018

0

Kwa habari za Papo kwa papo Simba,yanga na Nyingine Like Ukurasa wetu wa facebook HAPA

Barcelona Mabingwa Super Cup 2018

Klabu ya Barcelona, imetwaa ubingwa wa kombe la Super Cup,kwa kuifunga Sevilla kwa magoli 2-1 katika mchezo uliochezwa nchini Morroco.

Sevilla ndio walianza kuzifumania nyavu za wapinzani wao kwa kufunga goli ka kuongoza katika dakika ya tisa ya mchezo kupitia kwa mchezaji wake Pablo Sarabia.

Beki kisiki wa Barcelona, Gerald Pique, akasawazisha goli hilo katika dakika ya 42 ya mchezo, winga wa Kifaransa Ousmane Dembele,akaifungia timu yake bao la ushindi katika dakika ya 78.

Golikipa wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, aliibuka shujaa katika mchezo huo kwa kuokoa mkwaju wa penati wa dakika za lala salama ulipigwa na mchezaji wa Sevilla, Wissam Ben Yedder.

Barcelona wamecheza michezo tisa kati ya kumi ya Super Cup na huu ukiwa ni mchezo wa kwanza kupatikana bingwa kwa kuchezwa mchezo mmoja na mchezo ukichezwa nje ya nchi ya Hispania.

Punguza matumizi ya MB downoload App Bora ya Michezo BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY