CAF yatoa majibu ya Uchunguzi Waamuzi wanne wa Tanzania

CAF yatoa majibu ya Uchunguzi Waamuzi wanne wa Tanzania

0

CAF yatoa majibu ya Uchunguzi Waamuzi wanne wa Tanzania

Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) limetoa majibu ya uchunguzi wa waamuzi wanne wa Tanzania waliofikishwa kwenye Shirikisho hilo kufuatia kuripotiwa kwa vurugu kwenye hoteli waliyofikia nchini Burundi walipokwenda kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Africa.

Waamuzi waliokuwa wakichunguzwa kuhusishwa na ripoti ya mchezo huo kati ya Lydia Ludic ya Burundi na Rayon ya Rwanda ni Soud Idd Lila, Frank John Komba, Mfaume Ali Nasoro na Israel Mujuni.

Ilidaiwa kuwa katika hoteli waliyofikia kulitokea vurugu kwa madai kuwa moja ya timu hizo mbili ilitaka kupanga matokeo kupitia waamuzi hao.

CAF katika taarifa yake iliyosainiwa na Katibu Mkuu Amr Fahmy imesema waamuzi hao wa Tanzania wako safi hakuna jambo lolote baya linalowazunguka kuhusiana na mchezo huo uliochezwa February 21,2018 Uwanja wa Prince Louis Rwagasore,Burundi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY