CV ya Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike toka Nigeria

CV ya Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike toka Nigeria

0

CV ya Kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike toka Nigeria

Emmanuel Amunike ni jina la kocha mpya wa Timu ya TAIFA YA TANZANIA, Taifa Stars ni raia wa Nigeria akiwa alizaliwa 25 December 1970 huko Ezibodo Nigeria.

Wakati akicheza soka  kwenye timu ya Taifa ya Nigeria na vilabu mbalimbali alikuwa akicheza nafasi ya winga (Kiungo wa pembeni)

Katika maisha yake ya soka alifanikiwa kuchukua ubingwa katika ligi ya Nyumbani kwao nchini Nigeria na Nchini Misri katika vilabu vya Julius Berger Fc ya Nigeria  na Zamalek ya Misri.

Akicheza katika klabu ya Zamalek ya Misri (1991-1994) alifanikiwa kucheza jumla ya mechi 71 Huku akifunga jumla ya magoli 26.

Baadaye 1994 – 1996 alijiunga na soka la Kulipwa nje ya bara la Afrika katika nchi ya Ureno barani Ulaya ambapo alicheza katika klabu ya Sporting CP  AMBAPO alifanikiwa kucheza jumla ya mechi 51 na Kufunga magoli 17.

1996 – 2000 ALICHEZA katika klabu ya Barcelona ya nchini Hispania na alifanikiwa kucheza jumla ya mechi 19 pekee  ambapo alifunga bao 1 pekee.

Baadae alienda katika klabu ya Albacete iliyokuwa inashiriki Segunda Division huko Hispania kutoka  2000 hadi 2002,  na baadaye akaondoka barani ulaya mpaka Korea kusini katika klabu ya Busan I’cons mwaka 2003.

Baadaye aliamua kumalizia soka lake katika klabu ya Al Wehdat ya Jordan katika msimu wa 2003-2004.

KATIKA NGAZI YA TIMU YA TAIFA.

Emmanuel Amunike anamafanikio makubwa katika timu ya Taifa ya Nigeria, Kwanza kabisa akiwa amecheza jumla ya mechi 27 toka mwaka 1993 – 2001 na alifanikiwa kufunga jumla ya magoli 9.

Katika mwaka 1994 alikuwa ni moja ya wachezaji wa Kikosi cha Nigeria kilichoshiriki kombe la Dunia huko nchini Marekani akiisaidia Nigeria kupata ushindi mbele ya Bulgaria (Nigeria 3-0 Bulgaria) na Mechi dhidi ya Italia (Italia 1 – 2 Nigeria)

Na katika mwaka huo huo akiwa timu ya Taifa ya Nigeria aliisaidia Nigeria kutwaa taji la bingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) Michuano iliyofanyika huko Nchini Tunisia.

Mwaka 1994 msomaji wa Kwataunit.co.ke unaweza ukasema ulikuwa mwaka wake wa Mafanikio zaidi katika soka kwani katika mwaka huo alifanikiwa kuwa Mchezaji bora barani Afrika.

AKIHUDUMU KAMA KOCHA

Akihudumu kama Kocha Emmanuel Amunike alianza 2008 kama Kocha msaidizi wa Al Hazm, Na kisha 2008-2009 akawa kocha wa klabu yake ya zamani ya huko Nigeria Julius Berger, 2009 – 2011 akafundisha Ocean Boys nayo ya Nigeria

Mwaka 2014-2017 akawa kocha wa Nigeria chini ya Miaka 17, na 2017-2018 akaifundisha klabu ya Al Khartoum Sc.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY