Emmanuel Martin ataja wawili wapya Yanga walioongeza Nguvu Kikosini

Emmanuel Martin ataja wawili wapya Yanga walioongeza Nguvu Kikosini

0

Emmanuel Martin ataja wawili wapya Yanga walioongeza Nguvu Kikosini

Kiungo wa Klabu ya Yanga Emmanuel Martin amefunguka Juu ya Kile kinachoendelea ndani ya Kambi ya Yanga iliyopo mkoani Morogoro, Yanga ikijiandaa na Michuano mbalimbali.

Emmanuel Martin amesema Ujio wa Mrisho Ngassa na Mshambuliaji raia wa Congo Heritier Makambo umeongeza sana nguvu hasa kwenye safu ya Ushambuliaji ya Yanga.

Emmanuel Martin amesema Heritier Makambo ni mchezaji mwenye kasi uwanjani na anauwezo mkubwa wa Kufumania Nyavu hivyo kama moto wake atauhamishia kwenye ligi basi Yanga itakuwa ya Moto.

Kuhusu Mrishio Ngassa Emmanuel Martin amefunguka na Kusema Nyota huyo bado hajaisha kama watu wanavyosema kwani amekuwa akionyesha uwezo mkubwa awapo mazoezini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY