Habari mpya kutoka Yanga leo 15.8.2018

Habari mpya kutoka Yanga leo 15.8.2018

0

Habari mpya kutoka Yanga leo 15.8.2018

Klabu ya Yanga bado iko mkoani Morogoro ikijiandaa na mchezo dhidi ya USM Alger Agosti 19, 2018 katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Mpaka sasa Yanga imecheza michezo mitatu ya Kirafiki dhidi ya Tanzanite Academy ikishinda 5 kwa 1, Dhidi ya Mawenzi Market ikishinda 1 kwa 0 na Kisha kucheza na Kilosa Combine ambapo ilishinda 1 kwa 0 pia.

Leo 15.8.2018 kikosi cha Yanga kitashuka dimbani kucheza na Mkamba Rangers ya Mkoani Morogoro timu inayoshiriki ligi daraja la Pili mchezo ambao utachezwa kuanzia majira ya saa kumi kamili alasiri katika uwanja wa CCM Mkamba mkoani Morogoro.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY