Habari mpya kutoka Yanga leo 27.8.2018

Habari mpya kutoka Yanga leo 27.8.2018

0

Habari mpya kutoka Yanga leo 27.8.2018

IKUFIKIE hii mpya nyingine kutoka katika klabu ya Yanga yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar Es Salaam.

Ikiwa leo Yanga inatarajiwa kukwea pipa kwenda nchini Rwanda katika jiji la Kigali kuna Taarifa ya Kocha wao Mwinyi Zahera kocha raia wa Congo.

Kocha huyo baada ya mechi kati ya Rayon Sports na Yanga hatarejea na Kikosi cha Yanga nchini Tanzania na badala yake ataunganisha ndege kuelekea Congo.

Kocha huyo ataelekea Congo kwenye majukumu ya timu ya Taifa ambapo yeye ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo ambapo anatarajiwa kukaa huko kwa siku kadhaa akiiandaa timu ya Taifa ambayo inajiandaa na mchezo dhidi ya Liberia.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY