Habari mpya na Njema kutoka Yanga leo 11.8.2018

Habari mpya na Njema kutoka Yanga leo 11.8.2018

0

Kwa habari za Papo kwa papo Simba,yanga na Nyingine Like Ukurasa wetu wa facebook HAPA

Habari njema kwa Yanga leo Jumamosi 11.8.2018

Klabu ya Yanga ya Jijini Dar Es Salaam inaendelea na maandalizi ya msimu wa 2018/2019 na mchezo wa kimataifa kombe la shirikisho barani Afrika CAF dhidi ya USM ALger.

Kuelekea hayo Yote klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano amekuja na habari ambazo ni njema kwa wana Yanga.

CANNAVARO ATAENDELEA KULA MASHAVU YANGA

Katika wachezaji ambao ama kwa hakika ni vipenzi kwa watu wa Yang basi ama kwa hakika Nadir Haroub Cannavaro ni moja ya wachezaji hao akicheza kwa muda mrefu lakini Pia akitwaa mataji mengi akiwa na Yanga.

Basi Yanga msomaji wa Kwataunit.co.ke wameamua Cannavaro asiishie kuwa meneja tu wa Klabu hiyo ya Yanga na badala yake kwa sasa wanafikiria kumsomesha ili baadaye awe kocha wa kuweza kuisaidia Yanga.

Kwasasa wanachosubiri Yanga ni endapo tu itatokea kozi ya Ukocha basi Cannavaro atakuwa anaingia shule kuanza kusomea Kozi za Ukocha.

MIPANGO YA KUSTAAFISHA JEZI NAMBA 23.

Kutokana na heshima na mafanikio makubwa ndani ya Yanga kuna taarifa za Uhakika kuwa Yanga wapo katika mipango ya kustaafisha jezi namba 23 ambayo alikuwa anaivaa Nadir Haroub Cannavaro.

MAENDELEO YA MATHEO ANTHONY MAMBO MAZURI.

Baada ya kuelezwa kuwa mshambuliaji Matheo Anthony aliumia na Yanga ikicheza mchezo wa Kirafiki na Morogoro Tanzanite Academy Nyika amefunguka kuwa hayakuwa maumivu makubwa sana na kwasasa anaendelea vizuri

Punguza matumizi ya MB downoload App Bora ya Michezo BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY