Habari nyingine njema kutoka Simba leo 16.8.2018

Habari nyingine njema kutoka Simba leo 16.8.2018

0

Habari nyingine njema kutoka Simba leo 16.8.2018

Simba mambo yanaendelea kuwanyookea huku kila kitu kikionekana kwenda kwenye mstari ulionyooka, Achana na ushindi wa jana dhidi ya Arusha United wakicheza mjini Arusha kwenye mchezo wa Kirafiki.

Kaimu rais wa Simba Salim Abdallah Try Again amefungukuka kuwa jana klabu hiyo ilifanya ziara bandarini kwenda kuangalia zile nyasi zao zilizozuiliwa

Lengo la kufanya ziara hiyo ilikuwa ni kuziangalia nyasi hizo za Bandia kama bado zinaubora unaotakiwa na katika ukaguzi huo walizikuta nyasi hizo zikiwa bado ni bora

” Mipango iko mbioni na nafikiri ndani ya wiki mbili nyasi hizo zoezi la kuzichukua litakuwa limekamilika hivyo kuruhusu mipango mingine ya Ujenzi wa Uwanja Itaendelea “

Simba waliweka wazi kuwa udhamini walioupata kutoka katika kampuni ya A1 Chini ya Brand ya Mo Energy kiasi cha milioni 250 zitapelekwa kwenye ujenzi wa Uwanja wao wa Bunju.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY