Hizi ndizo sababu 2 zinazotajwa Kumng’oa Masoud Djuma Simba

Hizi ndizo sababu 2 zinazotajwa Kumng’oa Masoud Djuma Simba

0

Hizi ndizo sababu 2 zinazotajwa Kumng’oa Masoud Djuma Simba

Ukiachana na Simba kuwa na  mchezo dhidi ya Mbeya City leo kuanzia majira ya saa kumi na mbili jioni habari nyingine ya Kushtua ambayo inasambaa ni Simba kuvunja mkataba na Kocha wake Masoud Djuma raia wa Burundi.

Taarifa ambazo zimeandikwa na Gazeti la Champion la nchini Tanzania zinaeleza kuwa kamati mbili ile ya Utendaji na Ile ya Bodi bodi ya Wakurugenzi imekuwa Ikimjadili kocha huyo katika vikao vilivyoanza Alhamis mpaka Jumamosi na Kufikia maamuzi ya kuamua Kuvunja naye Mkataba.

Mambo hayo mawili yanayotajwa Kumng’oa kocha huyo ni Kushawishi wachezaji kucheza chini ya Kiwango ili kocha Patrick Aussems afukuzwe lakini pia tabia ya Masoud Djuma kutoelewana na Makocha wote wakuu wa Klabu ya Simba akianza na Pierre Lechantre na Wasasa Patrick Aussems.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Masoud Djuma amekuwa na kikundi cha wachezaji ambao anaelewana nao na ndiyo amekuwa akiwashawishi kutocheza kwenye Kiwango cha Juu ili kumtibulia kocha Mkuu, Kwahiyo vikao vya Kamati hizo 2 vimeamua Kuachana naye na Muda wowote ule wanaweza kutangaza juu ya maamuzi hayo. kupata zaidi habari Exclusive za Simba like Ukurasa wetu wa Facebook HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY